Rais Xi Jinping atoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa wachina wote
2023-01-20 18:47:12| cri

Rais Xi Jinping wa China kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Baraza la serikali la China ametoa salamu za mwaka mpya wa jadi kwa Wachina wote kwenye sherehe iliyofanyika leo mjini Beijing.

Rais Xi Jinping ambaye pia katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC na mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Kijeshi ya Chama, alitoa hotuba kwenye mkutano uliofanya kwenye Jumba la mikutano ya Umma, akiwasalimu wachina wa makabila yote, ndugu wa Hong Kong, Macao na Taiwan, na Wachina wanaoishi ng'ambo.

Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi ya China ambayo pia hufahamika kama sikukuu ya Spring, imeangukia Januari 22 mwaka huu.