Mashirika ya biashara ya Zimbabwe kuandaa kongamano la kupiga jeki mahusiano ya biashara na China
2023-01-20 08:51:59| CRI

Mashirika ya biashara, utalii na uwekezaji ya Zimbabwe yanapanga kuandaa kongamano la biashara kwa ajili ya kupiga jeki biashara na uwekezaji na China.

Mkurugenzi mwendeshaji wa shirika la kukuza biashara ZimTrade, Similo Nkala amesema China imekuwa mshirika muhimu wa Zimbabwe, na juhudi zaidi zitafanywa ili kupiga chapuo uhusiano kati ya nchi mbili. Nkala amesema Zimbabwe itaongeza shughuli za kurahisisha biashara na kupanua upatikanaji wa bidhaa zake kwenye masoko tofauti kama vile ya China, Malaysia na Misri. Akitolea mfano China, amesema ikiwa kama mwagizaji mkubwa na kujivunia kwa kuwa na watu wengi, soko hili linakuwa moja ya masoko makuu ya uagizaji ya Zimbabwe, na tayari lipo nafasi ya tatu kama muagizaji mkubwa wa bidhaa za Zimbabwe.

China na Zimbabwe zilisaini mkataba wa kununua machungwa mwaka 2022, na kuyapa fursa makampuni ya nchi hiyo kusafirisha machungwa nchini China, ambayo ni moja ya watumiaji wakubwa wa bidhaa za machungwa duniani.