Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa atuma salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa Wachina
2023-01-20 15:53:57| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma salamu za Mwaka Mpya wa Jadi wa China kwa Wachina, akiishukuru China kwa uhusiano wake imara na Umoja wa Mataifa na uungaji mkono wa ushirikiano wa kimataifa.

Katika ujumbe wake kwa njia ya video, Bw. Guterres amesema anafurahi kutuma salamu hizo za Mwaka wa Sungura, akisema Sungura ni alama ya bidii na unyumbufu.

Mwaka Mpya wa Jadi wa China utaanza tarehe 22 mwezi huu.