Kundi la wanamgambo la CODECO lafanya shambulizi na kuua watu saba DRC
2023-01-20 08:49:52| CRI

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Farhan Haq Alhamisi alisema kundi la wanamgambo la CODECO liliripotiwa kuwaua watu saba kwenye kambi ya wakimbizi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Msemaji huyu alisema Tume ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) iliripoti kuwa shambulizi hilo lilitokea katika kambi ya wakimbizi ya Plaine Savo, kilomita 9 mashariki mwa Djugu mkoani Ituri. Walinzi wa amani wa UM wamechukua hatua mara moja ili kuhakikisha usalama wa kambi hiyo na kuzuia vurugu zaidi.