Maonesho ya taa ya CMG yafanyika mjini Addis Ababa
2023-01-21 17:10:38| cri

Maonesho ya taa ya Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG kwa kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China yalifanyika tarehe 20 usiku katika jengo la makao makuu ya Benki ya Biashara ya Ethiopia mjini Addis Ababa.

Hii ni mara ya kwanza kwa CMG kuandaa maonesho ya taa ya kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China katika nchi ya Afrika. China na Ethiopia zina urafiki na ushirikiano wa muda mrefu. Jengo la makao makuu ya Benki ya Biashara ya Ethiopia mjini Addis Ababa lilijengwa na Kampuni ya Ujenzi ya China CSCEC, lina urefu wa mita 209.15 na ni jengo refu zaidi katika eneo la Afrika ya Mashariki.

Katika miaka ya hivi karibuni, Waethiopia wengi zaidi wana hamu kubwa ya kujua utamaduni wa China. Hivyo licha ya maonesho ya taa, tarehe 22 Januari CMG pia itaonesha baadhi ya vipindi vya tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China kwenye uwanja wa Meskel ambao ni uwanja mkubwa zaidi nchini Ethiopia.