Tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China latoa "Chakula cha jioni cha Kitamaduni cha Mwaka Mpya" kwa watu wa China kote duniani
2023-01-21 20:16:42| cri

Saa 2 usiku wa tarehe 21 Januari, likiambatanishwa na wimbo unaoimbwa na watoto, tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China ambalo limeandaliwa na Shirika kuu la utangazaji la China CMG limerushwa hewani, na kutoa "Chakula cha jioni cha Kitamaduni cha Mwaka Mpya" kwa watu wa China kote duniani.

Wakati huu, mamia ya mamilioni ya watazamaji kote duniani wanaketi mbele ya televisheni au kupitia new media, kutazama tamasha hilo moja kwa moja kwa pamoja. Tamasha hilo limetambuliwa na Rekodi ya Guinness, likiwa ni tamasha linalotazamwa na watu wengi zaidi duniani kupitia televisheni.

Mwaka 1983, kituo cha taifa cha televisheni cha China CCTV kiliandaa tamasha la kwanza la sanaa na utamaduni la mwaka mpya wa jadi wa China , liitwalo “Chunwan. Kila ifikapo mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China, wanafamilia kukusanya kukaa pamoja kutazama tamasha hilo imekuwa ni desturi ya watu wa China, pia limekuwa “Chakula cha jioni cha Kitamaduni cha Mwaka Mpya” kwa watu wa China kote duniani.

Tamasha hilo la mwaka 2023 limejumuisha utamaduni wa jadi wa China, Maisha halisi na ustaarabu wa nchi mbalimbali duniani, likitumia njia za Sanaa za kisasa, na uvumbuzi wa teknolojia mbalimbali za mwanga na kivuli, linajumuisha maonesho ya nyimbo na ngoma, mazingaombwe, opera, Wushu, sarakasi na vipindi vya aina mbalimbali.

Katika mwaka uliopita watu wa kawaida nchini China wamefanya juhudi sana. Kama rais Xi Jinping alivyosema kwenye salamu za mwaka mpya, “si rahisi kwa kila mtu”. Tamasha la mwaka huu linazingatia zaidi watu wa kawaida na hisia zao.