Katibu Mkuu wa UNCTAD: China yaleta habari nzuri duniani
2023-01-21 17:06:40| cri

Kwenye mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia wa mwaka 2023, Katibu Mkuu wa UNCTAD Bi. Rebecca Greenspan amesema maendeleo na ufunguaji mlango wa China umeleta habari njema kwa dunia.

Bi. Greenspan amesisitiza kuwa utengano wa biashara haufai kwa maendeleo ya kimataifa. Dunia inahitaji China na Marekani kuwa sehemu ya pamoja ya mfumo wa uchumi wa dunia, ambao ni muhimu kwa nchi zinazoendelea.

Amesema Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" la China linaweza kuongeza nguvu ya uzalishaji kwa nchi zinazoendelea na kuzisaidia kuwa na viwanda na kubadilisha miundo yao ya uzalishaji.