Mkurugenzi Mkuu wa WTO: China ni injini ya ukuaji wa dunia
2023-01-22 18:09:38| CRI

Baraza la uchumi la Dunia la mwaka 2023 limefungwa huko Davos. Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Biashara Duniani (WTO) Bibi Ngozi Okonjo Iweala amesema baada ya kufungwa kwa mkutano huo kuwa Baraza la Uchumi la Dunia la mwaka huu limeikumbusha jumuiya ya kimataifa kwamba ushirikiano ambao haujawahi kutokea unapaswa kufanyika katika siku zijazo ili kutatua kihalisi matatizo yanayoikabili dunia ya sasa.

Bibi Iweala amesema China itarejesha mahitaji ya matumizi ya ndani, na sekta ya viwanda itarejea katika hali yake ya kawaida, hili ni jambo jema kwa uchumi wa dunia.

Akizungumzia sera za kujilinda kibiashara za baadhi ya nchi, Bibi Iweala amesema kuwa ushirikiano wa pande nyingi umeleta ustawi duniani, na utandawazi umewaondoa watu zaidi ya bilioni moja kutoka kwenye umaskini na kuleta ustawi kwa China, Ulaya, Marekani na sehemu nyingine nyingi, na China pia imepata maendeleo makubwa katika mchakato wa utandawazi.