Tamasha la mwaka mpya wa jadi wa China lililoandaliwa na CMG lafuatiliwa na watazamaji wengi wa ndani na nje
2023-01-22 18:22:32| cri

Tamasha la mwaka mpya wa jadi wa kichina lililoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG limewafikia watu bilioni 11.011 katika majukwaa yote ya vyombo vya habari, huku kiwango cha watazamaji vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 44 kikifikia asilimia 50.52. Kiasi cha maonesho ya moja kwa moja katika vyombo vipya vya habari na kufika katika nchi za nje kimeweka rekodi mpya ya kihistoria.

Channeli za lugha za kigeni za CGTN ikiwemo Kiingereza, Kifaransa, Kihispania, Kiarabu, Kirusi na majukwaa ya lugha 68 zikishirikiana na vyombo vya habari zaidi ya 1000 kutoka nchi na sehemu 173 ikiwemo, Marekani, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Hispania, Australia, Russia, Japan, Falme za Kiarabu, Singapore, Uturuki, Afrika Kusini na Kenya zimeonesha moja kwa moja au kuripoti kuhusu tamasha hilo. Aidha tamasha hilo limeoneshwa kwa mara milioni 42.72 kwenye channeli za CGTN na mara milioni 51.76 kwenye tovuti za mitandao ya kijamii ya CCTV.com, zikiongezeka kwa kiasi kikubwa ikilinganishwa na mwaka jana.