Maeneo maalum ya maendeleo ya China yachangia kutuliza biashara na nje na uwekezaji
2023-01-22 18:06:35| CRI

Wizara ya biashara ya China imesema maeneo ya maendeleo ya kiteknolojia ya ngazi ya taifa ya China yametajwa kuwa ni jukwaa muhimu la kufungua mlango, kutuliza biashara na nje na uwekezaji.

Mwaka 2021 biashara na nchi za nje iliyotathminiwa na wizara ya biashara kwenye maeneo 217 ya maendeleo, ilikuwa na thamani ya dola za kimarekani trilioni 1.3, ikichukua asilimia 22.8 ya biashara ya jumla na nchi za nje. Thamani ya biashara ya bidhaa za teknolojia ya juu kwa mwaka huo ilifikia yuan trilioni 3, na kuchangia zaidi ya robo thamani ya biashara ya bidhaa za teknolojia ya juu.

Uwekezaji wa moja kwa moja FDI uliotumika kihalisi kwenye maeneo hayo ulikuwa na thamani ya dola za Kimarekani bilioni 38.2, ukiwa ni asilimia 22 ya jumla ya uwekezaji huo kwa nchi nzima.