China yaendelea kupanua bima ya matunzo ya uzeeni
2023-01-22 18:05:59| CRI

Takwimu kutoka Wizara ya raslimali watu na uhakikisho wa jamii ya China zinaonesha kuwa watu wengi zaidi sasa wanaweza kujiunga na bima ya matunzo ya uzeeni, tangu usimamizi wa fedha za bima uboreshwe na kuwa chini ya usimamizi mmoja.

Hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, bima ya matunzo ya uzeeni nchini China ilikuwa imewafikia watu bilioni 1.05, watu milioni 24 zaidi kuliko mwaka juzi.

Chini ya utaratibu wa usimamizi mmoja wa bima, sera za pensheni zimeunganishwa katika nchi nzima ili haki na maslahi ya wafanyakazi na wastaafu viweze kulindwa vizuri zaidi.

Ofisa wa wizara ya rasilimali watu na uhakikisho wa jamii Bw. Qi Tao, amesema mwaka jana jumla ya Yuan bilioni 244 (Dola za Marekani bilioni 36) zilihamishwa katika ya mikoa mbalimbali ili kuunga mkono maeneo yenye changamoto ya kufanya malipo.