Nishati safi yachukua nafasi kubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati nchini China
2023-01-23 17:42:50| CRI

Umeme unaotokana na upepo na jua unachukua nafasi kubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme nchini China.

Takwimu zilizotolewa na Idara ya Taifa ya Nishati (NEA) ya nchini China zimeonyesha kuwa, mwaka jana, umeme unaotokana na jua na upepo ulifikia kilowatii milioni 120, na jumla ya umeme uliowekezwa ulipita kilowati milioni 700 mpaka kufikia mwisho wa mwaka jana.

Idara hiyo imesema, umeme wa jua umetoa mchango mkubwa katika kutuliza usambazaji wa umeme katika mikoa inayotoa umeme wa nguvu ya jua, ikiwemo mkoa wa Jiangsu na Zhejiang, wakati wa kilele cha msimu wa joto mwaka jana.