Idara ya Taifa ya Takwimu ya China (NBS) imesema, jumla ya matumizi ya China katika utafiti na maendeleo (R&D) kwa mwaka jana ilifikia karibu dola za Marekani bilioni 456, ambayo imeongeza kwa asilimia 10.4 kuliko mwaka 2021.
Baada ya kutoa vipengele vya bei, matumizi ya utafiti na maendeleo ya China mwaka jana yaliongezeka kwa asilimia 8 kwa kulinganishwa na mwaka juzi. Na jumla ya matumizi ya China katika utafiti na maendeleo yalichukua asilimia 2.55 ya pato la taifa mwaka jana, ikiongeza kwa asilimia 0.12 ikilinganishwa na mwaka 2021.