Tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa sungura na tamasha la mwanga yaliyoandaliwa na CMG yaonyeshwa barani Afrika
2023-01-23 17:45:11| CRI

Tamasha la Mkesha wa Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina na shughuli husika zilizoandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) limeletea mazingira ya furaha barani Afrika.

Tarehe 20 mwezi huu, Tamasha la Mwanga lililoandaliwa na CMG kukaribisha sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa China lilionyeshwa nchini Ethiopia, na kulifanya jengo la makao makuu ya Benki ya Biashara ya Ethiopia ling’are wakati wa usiku na kuvutia watembeleaji wengi kupiga picha.

Nchini Afrika Kusini na Kenya, tamasha la Mkesha wa Mwaka Mpya wa Jadi wa Sungura wa China lilionyeshwa moja kwa moja usiku wa tarehe 21 mwezi huu. Tamasha hilo sio tu limewaburudisha Wachina walioko katika nchi hizo katika sikukuu hiyo maalumu, bali pia limefanya utamaduni wa China ueleweka zaidi kwa watu wa Afrika.