Rais wa Ufaransa ataka nchi hiyo na Ujerumani kuwa waasisi wa msingi mpya wa Ulaya
2023-01-23 17:44:05| CRI

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema nchi yake na Ujerumani zinapaswa kuwa waasisi wa msingi mpya wa Ulaya.

Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 60 ya upatanisho wa Ujerumani na Ufaransa jana jumapili mjini Paris, rais Macron amesema jukumu la kwanza la nchi hizo mbili, kama waasisi, linapaswa kuwa kujenga kwa pamoja mfumo mpya wa nguvu usioangalia tofauti zao.

Kwa upande wake, Kansela wa Ujerumani Olaf Scholtz amesema, hatma ya Ulaya inategemea nguvu ya msukumo ya Ujerumani na Ufaransa.

Pis jumapili, Baraza la Mawaziri wa Ujerumani na Ufaransa lilikutana, na mada mbalimbali ikiwemo uchumi, uhamishaji wa nishati, ulinzi na sera za Ulaya zilijadiliwa.