Zambia kushitikiana na China katika siplomasia ya michezo
2023-01-24 17:39:21| CRI

Katibu mkuu wa Idara ya Michezo na Vijana katika Wizara ya Vijana, Michezo na Sanaa nchini Zambia, Kangwa Chileshe amesema, China ni moja ya nchi za kigeni ambayo Zambia inahusiana nayo katika siplomasia ya michezo na miradi ya kubadilishana uzoefu ili kuwezesha ujasiriamali kati ya vijana nchini humo.

Katika mahijiano na Shirika la Habari la China Xinhua, Bw. Chileshe amesema serikali ya Zambia imejizatiti katika kushirikiana na China katika maendeleo ya michezo. Ameongeza kuwa, Wizara ya Mambo ya Nje na Usalama wa Ndani zimeandika barua kwa balozi za nchi hiyo nje ya nchi kuhusu kuanza kutekeleza diplomasia ya michezo na kubadilishana uzoefu.

Amesema mpaka sasa China imejenga viwanja viwili vikubwa vya michezo nchini Zambia, na kwamba serikali ya nchi hiyo imetaka China kufikiria kuhusu kufanya ukarabati wa viwanja hivyo.