Jeshi la Majini la Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa mazoezi ya kijeshi na China na Russia
2023-01-24 17:37:45| cri

Wizara ya Ulinzi na Maveterani wa Kijeshi ya Afrika Kusini imesema, nchi hiyo itakuwa mwenyeji wa vikosi vya jeshi la majini kutoka China na Russia wakati wa mazoezi ya kijeshi ya kimataifa yaliyopangwa kufanyika mwezi ujao huko Durban na Pwani ya Richards mkoani KwaZulu-Natal.

Taarifa iliyotolewa na wizara hiyo imesema, mazoezi hayo yanayojulikana kama Mosi II yatafanyika kuanzia Februari 17 hadi 27, na zaidi ya wanajeshi 350 wa Afrika Kusini wataungana na wenzao kutoka China na Russia katika mazoezi hayo.