Burkina Faso yathibitisha kusimamisha makubaliano ya kuwepo kwa jeshi la Ufaransa nchini humo
2023-01-24 17:39:58| CRI

Serikali ya Burkina Faso imethibitisha kuwa imeiambia Ufaransa kuondoa askari wake walioko nchini humo ndani ya mwezi mmoja, na kusema hatua hiyo inaendana na masharti ya makubaliano.

Msemaji wa serikali ya Burkina Faso Jean-Emmanuel Ouedraogo amesema hatua hiyo ni ya kawaisa kwa kuwa imeelekezwa katika masharti ya makubaliano ya kijeshi ambayo yanaruhusu uwepo wa askari wa Ufaransa nchini humo.

Hata hivyo, msemaji huyo amehakikisha kuwa kuwa hatua hiyo haihusiani na tukio lolote mahsusui, lakini linahusiana na nia ya mamlaka za mpito na kuungwa mkono na wananchi wa nchi hiyo.

Uamuzi huo umekuja wakati serikali ya Burkina Faso inakabiliwa na maandamano yanayodai kuondolewa kwa askari wa Ufaransa nchini humo.