Jeshi la Somalia laua wapiganaji 39 wa kundi la al-Shabab katikati ya nchi hiyo
2023-01-24 17:41:29| CRI

Jeshi la Somalia jana limewaua wapiganaji 39 wa kundi al-Shabab baada ya mapigano makali yaliyotokea karibu na mji wa Harardhere.

Kamanda wa askari wa miguu wa nchi hiyo Mohamed Tahlil Bihi amekiambia kituo cha Radio Mogadishu kuwa, wapiganaji hao waliouawa walichoma moto basi moja la abiria wakati walipotoroka kwenye mapigano.

Mapigano hayo yalitokea siku moja baada ya kundi hilo kufanya shambulizi baya katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu Jumapili iliyopita.