Rais Xi ahutubia Mkutano wa Kilele wa Saba wa CELAC
2023-01-25 17:26:18| CRI

Mkutano wa Kilele wa Saba wa Nchi za Latini America na Caribbean (CELAC) ulifanyika Jumanne huko Buenos Aires, nchini Argentina. Kutokana na mwaliko wa rais wa Argentina Alberto Fernandez ambaye ni mwenyekiti wa zamu wa CELAC, rais Xi Jinping wa China alihutubia mkutano huo kwa njia ya video.

Katika hotuba yake rais Xi amesema nchi za Latini America na Caribbean ni wanachama muhimu wa nchi zinazoendelea. Pia wameshiriki kikamlifu katika utawala wa dunia na kutoa mchango muhimu. Amebainisha kuwa CELAC imekuwa chachu kubwa katika ushirikiano wa Kusini na Kusini, na kwamba imebeba jukumu muhimu katika kulinda amani ya kikanda, kuhimiza maendeleo ya pamoja na kuboresha mafungamano ya kikanda, hivyo rais Xi amesisitiza kuwa China siku zote inaunga mkono mchakato wa mafungamano ya kikanda ya Latini America na Caribbean.

Ameongeza kuwa China iko tayari kuendelea kushirikiana na nchi za LAC kusaidiana na kupata maendeleo kwa pamoja, na kutetea “amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru”.