Qin Gang atoa salamu ya rambirambi kwa wizara ya mambo ya nje ya Gabon juu ya kifo cha waziri Adamo
2023-01-25 17:27:17| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Qin Gang ametoa salamu za rambirambi kupitia simu kwa wizara ya mambo ya nje ya Gabon kutokana na kifo cha waziri Michael Moussa Adamo.

Katika salamu zake Bw. Qin pia amewapa pole jamaa wa waziri huyo. Adamo ni mwanasiasa na mwanadiplomasia muhimu wa Gabon, ana urafiki mkubwa na uhusiano mzuri na watu wa China, ambapo alihimiza urafiki kati ya nchi mbili na kutoa mchango mkubwa katika maendeleo ya uhusiano huo. Aidha Bw. Qin amesema China inapenda kufanya juhudi pamoja na Gabon, ili kuhimiza ushirikiano wa nchi mbili kuzidi kupata maendeleo mengi zaidi.