Abiria wanaotumia treni ya SGR nchini Kenya kuanza kununua tiketi bila kutumia pesa taslimu
2023-01-26 17:25:31| cri

Abiria wanaotumia treni ya SGR nchini Kenya, kuanzia Februari Mosi watakuwa wakilipia huduma kwa kutumia simu za mkononi ama kwa kadi za kielektroniki ili kuongeza ufanisi.

Kwenye tangazo lake lililotoa Jumanne jioni, Shirika la Reli la Kenya lilisema treni hiyo, ambayo imeanza kufanya kazi tangu mwaka 2017, kwa miaka mingi imekuwa ikitumia mfumo wa malipo mseto ambao unahusisha pesa taslimu, peza za simu na kadi za kielektroniki.

Reli ya SGR iliyojengwa na China inabeba jukumu muhimu katika kupiga jeki ukuaji wa uchumi wa Kenya, na idadi ya abiria wanaotumia treni ya SGR imekuwa ikiongezeka.