Mjumbe wa China ahimiza mwitikio mzuri wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Sudan
2023-01-26 17:28:14| CRI

Konsela wa Ujumbe wa Kudumu wa China katika Umoja wa Mataifa Bw. Liang Hengzhu ametoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuitikia vyema kuhusu kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Sudan.

Bw. Liang amesema hayo kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la UM, akiongeza kuwa kujenga upya utawala wa sheria na kupata haki huko Darfur nchini Sudan ni malengo ya pamoja ya jumuiya ya kimataifa. Alifahamisha kuwa kutekeleza Makubaliano ya Amani ya Juba na kujenga uwezo wa kimahakama wa serikali ya Sudan kunahitaji usaidizi wa kifedha. Jumuiya ya kimataifa inapaswa kutozingatia masuala ya kisiasa na kutoa msaada unaoonekana kwa Sudan.

Amesisitiza kuwa msimamo wa China kuhusu ushiriki wa Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa ICC nchini Sudan bado haujabadilika. China inatumai kwamba Mahakama hiyo itazingatia kikamilifu kanuni ya mamlaka inayokamilishana na kuheshimu kwa dhati mamlaka ya mahakama ya Sudan.