AfDB kuingiza dola bilioni 10 katika mamlaka ya chakula ya nchi za Afrika
2023-01-26 17:46:51| CRI

Mkuu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina Jumatano mjini Dakar, Senegal alitangaza kuwa Benki hiyo itatoa hadi dola za Kimarekani bilioni 10 kwa maendeleo ya kilimo na mamlaka ya chakula katika bara la Afrika.

Mkuu huyo wa AfDB alitoa tangazo hilo katika ufunguzi wa awamu ya pili ya Mkutano wa Dakar kuhusu Mamlaka ya Chakula. Alisema ufadhili huu utatumiwa kuunga mkono utoaji wa pembejeo za kilimo na chakula moja kwa moja. Pia alisema kile Afrika inachofanya katika kilimo ndicho kitakachoamua ugavi wa chakula duniani. Mataifa mengine yataunga mkono Afrika katika kufikia malengo yake.

Akinwumi Adesina alieleza kuwa Mkutano wa Dakar lazima uanzishe "mwanzo mpya kuelekea lengo jipya," akisisitiza kuwa asilimia 65 ya ardhi inayolimwa duniani iko barani Afrika. Anasikitika kuona bara la Afrika likitegemea kuagiza bidhaa kutoka nje na ukweli kwamba mamilioni ya Waafrika wanalala njaa.