China yataka majeshi ya kigeni kusimamisha uporaji wa maliasili nchini Syria
2023-01-26 17:11:53| cri

Naibu balozi wa China katika Umoja wa Mataifa, Bw. Dai Bing amesema uporaji wa maliasili nchini Syria unaofanywa na majeshi ya kigeni lazima ukomeshwe mara moja.

Akihutubia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Syria hapo jana, Bw. Dai alisema uwepo haramu wa wanajeshi wa kigeni na operesheni zao haramu za kijeshi nchini Syria lazima zikomeshwe, na kuongeza kuwa mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa Syria unapaswa kuheshimiwa.

Bw. Dai pia alisema, hali ya kukabiliana na ugaidi nchini Syria bado ni ngumu. Ameitaka jumuiya ya kimataifa kufuata sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama na kupambana na magaidi wote nchini Syria bila uvumilivu.