Takriban watu 20 wajeruhiwa katika shambulizi la bomu nchini DR Congo
2023-01-26 17:45:20| CRI

Takriban watu 20 walijeruhiwa Jumatano jioni kwenye shambulizi la bomu katika soko dogo mjini Beni, jimboni Kivu Kaskazini, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Msemaji wa jeshi la DRC katika eneo la Beni Kapteni Anthony Mwalushayi aliambia shirika la habari la China Xinhua kuwa kifaa cha kulipuka cha kienyeji kiliwekwa kwenye mfuko uliokuwa na mihogo karibu na mashine ya kusaga unga sokoni.

Wengi wa waliojeruhiwa ni wanawake waliokuwa wakiuza sokoni wakati kifaa hicho kilipolipuka. Takriban watu saba wamejeruhiwa vibaya.

Mwalushayi alisema, kwa sasa hakuna maelezo ya kutosha lakini vikosi vya usalama na huduma maalum zilifunga eneo la mlipuko kwa uchunguzi, na kuwabebesha lawama waasi wa ADF.