Rais Xi ampongeza Bob Dadae kwa kuchaguliwa tena kuwa gavana mkuu wa Papua New Guinea
2023-01-27 19:10:17| CRI

Rais Xi Jinping wa China amempongeza Bob Dadae kwa kuchaguliwa tena kuwa gavana mkuu wa Papua New Guinea (PNG).

Katika ujumbe wake, Xi alibainisha kuwa Papua New Guinea ni moja ya nchi za kwanza za visiwa vya Pasifiki kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya Watu wa China, na nchi hizo mbili zinafurahia kudumisha urafiki.

Xi alisema hivi sasa, ushirikiano wa kimkakati wa kina kati ya China na Papua New Guinea umekuwa ukiendelezwa kwa kiwango cha juu kwa kupata matunda mengi katika mawasiliano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na kuleta manufaa makubwa kwa watu wao.

Akielezea kutilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na PNG, rais Xi alisema yuko tayari kuendelea kufanya kazi na Dadae ili kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na kusonga mbele kwa maendeleo thabiti na endelevu ya uhusiano wa pande hizo mbili.