WFP yapokea dola milioni 71 za Kimarekani ili kushughlikia mzozo wa chakula katika Afrika
2023-01-27 17:25:19| cri

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limesema limepokea mchango wa dola milioni 71.44 za Kimarekani kutoka Umoja wa Ulaya ili kushughulikia mzozo wa chakula katika nchi 11 za Mashariki na Kusini mwa Afrika.

WFP limesema fedha hizo lilizopokea kupitia idara ya misaada ya kibinadamu, zimefanyiwa kazi mara moja katika kushughulikia mahitaji yasiyo ya kawaida ambayo yamesababishwa na athari za vita vya Ukraine, hali ya hewa, migogoro na shinikizo la kiuchumi.

Fedha hizo zitatumika kwenye operesheni za WFP nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Msumbiji, Rwanda, Somalia, Sudan Kusini, Sudan na Tanzania.