Sudan na Ethiopia zakubali kuondoa tofauti zao kupitia utaratibu wa pamoja na mazungumzo ya moja kwa moja
2023-01-27 17:24:09| cri

Sudan na Ethiopia zimekubali kuondoa mzozano wao wa mpaka pamoja na suala la Bwawa la GERD kupitia utaratibu wa pamoja na mazungumzo ya moja kwa moja.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Baraza la Utawala wa Mpito la Sudan Abdel Fattah Al-Burhan na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed katika mkutano uliofanyika Ikulu mjini Khartoum.

Al-Burhan alisisitiza haja ya kuongeza ushirikiano kati ya nchi mbili kwenye masuala ya pamoja, ya kikanda na kimataifa.

Naye Ahmed kwa upande wake, amesema Bwawa la GERD halitasababisha uharibifu wowote kwa Sudan, bali litanufaisha sekta ya umeme. Kuhusu suala la mpaka Ahmed amesema hilo ni suala la zamani na kuzitaka pande zote kurejea kwenye meza ya mazungumzo ili kulitatua.