Msemaji mkuu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Bw. Stephane Dujarric amesema, mashambulizi yaliyofanywa na waasi wa vuguvugu la M23 na mlipuko uliowajeruhi raia 18 umesababisha taharuki kubwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Bw. Dujarric amesema, mapigano ya kwanza yalitokea kusini mashariki mwa Kitchanga, katika jimbo la Kivu Kaskazini, wakati mapigano mengine, yakiwa ni pamoja na ya silaha nzito yalitokea Kishishe, takriban kilomita 25 kaskazini magharibi mwa Rutshuru katika jimbo hilo hilo.
Hivi sasa, walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanafanya doria za mara kwa mara kuzunguka kambi ya Umoja wa Mataifa huko Kitchanga na vijiji jirani ili kuzuia makundi yenye silaha kuleta madhara zaidi kwa raia.