Yemen yaunda vikosi vipya vya akiba kukabiliana na kundi la Houthi
2023-01-30 08:59:57| CRI

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Rais la Yemen (PLC) Rashad al-Alimi ametoa amri ya kuunda vikosi vipya vya akiba kwa ajili ya kupambana na kundi la Houthi.

Amri hiyo inahusu kuunda vikosi vinavyoitwa Ngao ya Taifa vilivyo chini ya usimamizi na uongozi wa rais ambaye ni kamanda mkuu wa jeshi la Yemen. Kutokana na amri hiyo Bw. al-Alimi ana majukumu kamili kuhusu vikosi hivi.

Bw. Al-Alimi pia ametoa amri nyingine ya kumteua Brigadier Bashir Saif Qaid al-Subaihi kuwa kamanda wa vikosi hivyo vipya.

Mapema mwezi huu, maofisa wa Yemen walisema pande hasimu nchini humo zinajiandaa kwa ajili ya duru mpya ya mapigano katika mwaka huu wakati kuna ukosefu wa hatua madhubuti za kuleta amani endelevu.