Wanamgambo 136 wa al-Shabab wauawa kusini mwa Somalia
2023-01-30 08:48:55| CRI

Naibu waziri wa habari wa Somalia Bw. Abdirahman Yusuf Al-adala amethibitisha kuwa vikosi vya usalama vya Somalia vimewaua wanamgambo 136 wa kundi la al-Shabab wakiwemo makamanda watatu wakuu katika operesheni maalum iliyotekelezwa kusini mwa Somalia Jumamosi usiku.

Bw. Al-adala amesema vikosi vya serikali vikiungwa mkono na washirika wa kimataifa viliendesha operesheni ya pamoja katika eneo la misitu karibu na mji wa Janale ambako magaidi hao walikuwa wamekusanyika.

Bw. Al-adala amewaambia wanahabari kuwa takriban wapiganaji 100 wa kundi la al-Shabab walijeruhiwa katika operesheni hiyo.