Rais wa Afrika Kusini aonya kuwa nchi hiyo haitaacha matumizi makaa ya mawe
2023-01-30 16:10:39| CRI

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa amesema nchi yake yenye utajiri wa makaa ya mawe lakini inakabiliwa na uhaba wa nishati, haitaacha mara moja mitambo yake ya kuzalisha umeme kwa kutumia visukuku inapohamia kwenye mifumo ya nishati safi.

Afrika Kusini, moja ya nchi zinazochafua zaidi mazingira duniani, inazalisha takriban asilimia 80 ya umeme wake kupitia makaa ya mawe, na licha ya hayo, inakabiliwa na uhaba mkubwa wa nishati.

Tangu mwaka 2021, nchi hiyo imepata mabilioni kadhaa ya dola katika mikopo ya kimataifa na ruzuku kusaidia mabadiliko ya kijani, lakini hata hivyo, rais Ramaphosa ameonya dhidi ya mtazamo kwamba wanapaswa kufanya biashara kati ya usalama wa nishati na mpito wa haki kuelekea uchumi wa chini wa kaboni.

Akiwahutubia maafisa wakuu wa chama tawala cha ANC, amesema haikuwa lazima kuchagua kati ya makaa ya mawe na nishati mbadala.