Tanzania yaanzisha programu ya kutokomeza ukoma kabla ya mwaka 2030
2023-01-30 08:28:10| CRI

Mamlaka za Afya za Tanzania jana ziliadhimisha Siku ya Kupambana na Ukoma Duniani na kutangaza programu mpya yenye lengo la kutokomeza ugonjwa huo nchini Tanzania kabla ya mwaka 2030.

Naibu waziri wa afya Bw. Godwin Mollel amesema programu hiyo inapanga kuwatambua wagonjwa wote wa ukoma nchini Tanzania, hali ambayo itaisaidia serikali kuwatibu wagonjwa hao na kudhibiti ugonjwa huo unaoathiri neva, ngozi, njia ya pua.

Amesema utambuzi wa ugonjwa huo utafanyika kutoka ngazi ya kijiji hadi ngazi ya mkoa ili kuwa na orodha ya wagonjwa hao. Programu hiyo pia itasaidia kutoa elimu kwa wafanyakazi wa afya na umma, kuhusu namna ya kudhibiti ugonjwa huo.