Watu 44 wameuawa kwenye mlipuko wa kujitoa mhanga mjini Peshawar, Pakistan
2023-01-31 09:07:12| CRI

Idadi ya watu waliouawa kwenye mlipuko wa mabomu uliotekelezwa na mshambuliaji wa kujitoa mhanga katika msikiti mmoja mjini Peshawar, magharibi-kaskazini mwa Pakistan imeongezeka na kufikia 44.

Msemaji wa hospitali ya Lady Reading ya huko amesema idadi hiyo inaweza kuongezeka kwani kati ya watu wasiopungua 157 waliojeruhuiwa, baadhi yao wako katika hali mbaya. Waliouawa ni pamoja na askari polisi, raia na Imam na wengine wasiopungua watatu kati yao bado hawajatambuliwa.

Ofisa mmoja amesema takriban watu 300 walikuwa kwenye sala katika msikiti huo wakati mlipuko unatokea.

Idara ya afya ya huko imetangaza hali ya dharura katika mji wa Peshawar na jeshi la ulinzi limeanza uchunguzi kuhusu tukio hilo.