Uchumi wa Ethiopia kukua kwa asilimia 7.5 katika mwaka huu wa fedha
2023-01-31 09:05:00| CRI

Waziri wa mipango na maendeleo wa Ethiopia Bw. Fitsum Assefa, amesema uchumi wa Ethiopia utakua kwa asilimia 7.5 katika mwaka huu wa fedha wa 2022/2023 ulioanza Julai 8.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na serikali ya Ethiopia, katika mwaka wa fedha uliopita wa 2021/2022, nchi hiyo ilirekodi ukuaji wa uchumi wa asilimia 6.4.

Waziri Assefa amesema viashiria vikuu vya kiuchumi vilivyorekodiwa katika miezi sita iliyopita, ni vya kutimizwa kwa makadirio ya ukuaji katika mwaka huu wa fedha.

Waziri huyo pia amesema sekta ya kilimo iko katika mstari wa kwanza katika kudumisha maendeleo ya uchumi wa nchi hiyo, huku akiongeza kuwa sekta hiyo imesajili ukuaji wa asilimia 6.7 katika miezi sita iliyopita.