Sudan yasisitiza ahadi kuhusu viwango vya kimsingi vya haki za binadamu
2023-01-31 09:13:33| CRI

Taarifa kutoka wizara ya mambo ya nje ya Sudan zinasema Sudan imesisitiza ahadi yake kuhusu vigezo vya kimsingi vya haki za binadamu.

Kaimu waziri wa mambo ya nje wa Sudan Bw. Ali Al-Sadiq alipokutana na mtaalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya haki za binadamu nchini Sudan Bw. Radhouane Nouicer, amesisitiza ushirikiano kati ya Sudan na Umoja wa Mataifa katika kuimarisha haki za binadamu nchini humo.

Bw. Nouicer amepongeza ushirikiano kati ya Sudan na mashirika ya kimataifa katika kuboresha haki za binadamu nchini humo. Amesisitiza kuwa Sudan inapaswa kufanya juhudi kutekeleza mpango wa kitaifa wa haki za binadamu.