Kenya iko mbioni kutokomeza magonjwa ya kitropiki yaliyosahaulika
2023-01-31 08:41:35| CRI

Waziri wa afya wa Kenya Bibi Susan Wafula amesema kazi ya kutokomeza Magonjwa ya Kitropiki Yaliyosahaulika (NTDs) imeshika kasi kwenye kaunti za mbali kufuatia ongezeko la uwekezaji kwenye kazi za kinga, tiba na matunzo.

Bibi Wafula amesema matumizi ya mifumo ya kimataifa pamoja na utoaji mkubwa wa fedha, mabadiliko ya kisera, usimamizi na mwamko kuhusu magonjwa hayo vitasaidia kutokomeza magonjwa hayo yanayoambukizwa kutokana na kung’atwa na wadudu.

Akiongea kwenye Siku ya Kupambana na Magonjwa ya Kitropiki Yaliyosahaulika katika kaunti ya Kisumu, Bibi Wafula amesema zaidi ya wakenya milioni 25 wako kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa hayo.

Shirika la Afya Duniani WHO limetaja magonjwa hayo kuwa ni hatari kwa afya.