Matukio ya ufyatuaji risasi yatokea mara kwa mara mwanzoni mwa mwaka huu
2023-01-31 23:40:17| cri

Kulingana na takwimu zilizotolewa tarehe 29 mwezi Januari na shirika la Marekani la Gun Violence Archive, matukio 44 ya ufyatuaji risasi kwa watu wengi yamerekodiwa nchini humo tangu mwaka huu uanze, idadi ambayo imekuwa kubwa zaidi kuliko miaka iliyopita kipindi kama hicho tokea mwaka 2014 shirika hilo lilipoanza kukusanya takwimu kama hizo. Kwa mujibu wa shirika hilo, mwaka 2022, matukio makubwa ya ufyatuaji risasi (mbali na mpiga risasi mwenyewe, angalau watu wanne waliuawa au kujeruhiwa) yamekuwa zaidi ya 600 kwa miaka mitatu mfululizo.