Namibia yarekodi kupungua sana kwa vitendo vya ujangili dhidi ya Tembo
2023-01-31 08:40:53| CRI

Wizara ya mazingira, misitu na utalii ya Namibia imesema vitendo vya ujangili dhidi ya Tembo nchini Namibia vimeendelea kupungua kwa kiasi kikubwa kuanzia mwaka 2015, na mwaka jana ni Tembo wanne tu waliouawa ikilinganishwa na Tembo 101 waliouawa mwaka 2015.

Hata hiyo msemaji wa wizara hiyo Bw. Romeo Muyunda amesema licha ya ujangili wa Tembo kupungua kwa kiasi kikubwa, ujangili wa Faru bado unaendelea kuwa juu, kwani mwaka jana Faru weusi 61 na weupe 26 waliuawa.

Bw. Muyunda amesema wizara yake na wadau wengine wa ulinzi wa mazingira na utekelezaji wa sheria wataimarisha juhudi za kupambana na uhalifu unaohusu wanyamapori hasa kupambana na ujangili wa Faru.