Tanzania ni miongoni mwa nchi ambazo uchumi unakadiriwa kuimarika mwaka 2023
2023-02-01 20:04:51| cri

Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo uchumi wake unakadiriwa kuimarika mwaka huu. Nchi tano zinazofanya vizuri kiuchumi barani humo zinatarajiwa kukua kwa zaidi ya asilimia 5.5 katika mwaka 2023/24.

Kwa mujibu wa ripoti ya AfDB iliyopewa jina la ‘Utendaji Bora wa Kiuchumi na Mtazamo wa Afrika’, uchumi wa Tanzania unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.6 mwaka huu. Nchi hiyo itaifuata Rwanda, ambayo uchumi wake unatarajiwa kukua kwa asilimia 7.9, ikifuatiwa na Côte d’Ivoire asilimia 7.1.

Uchumi wa Benin na Ethiopia katika kipindi cha (2023/24) utakua kwa asilimia 6.4 na 6 mtawalia. Makadirio ya AfDB yanaambatana na makadirio ya Benki ya Dunia kwamba uchumi wa Tanzania utapanuka kwa asilimia 5.3 mwaka 2023.