AfDB yaahidi kuunga mkono kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi barani Afrika
2023-02-01 09:06:07| CRI

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) itatoa raslimali zaidi kwa ajili ya kilimo kinachostahimili mabadiliko ya tabianchi barani Afrika, pia kutatua tatizo la uhaba wa chakula na kuongeza kipato vijijini.

Meneja wa sekta ya kilimo wa AFDB kanda ya Afrika Bw. Pascal Sanginga amesema benki hiyo imetenga fedha za ziada kuhakikisha wakulima wadogo wa Afrika wanapata ujuzi, teknolojia na pembejeo zinazohitajika kustahimili mabadiliko ya tabianchi.

Benki hiyo pia imeahidi kutoa dola za kimarekani wastani wa bilioni 2 kwa mwaka katika muda mfupi ujao kwa ajili ya kuhimiza kilimo cha aina hiyo kupitia kuboresha umwagiliaji, uvunaji wa maji, kuimarishwa kwa mawasiliano ya soko, kuboresha miundombinu na upatikanaji wa mbegu bora.