Wasichana zaidi ya elfu 9 wa shule za Tanzania wapata ujauzito ndani ya mwaka mmoja
2023-02-01 09:02:58| cri

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania, Bw. Omary Kipanga amesema wasichana 9,011 wa shule za Tanzania walipata ujauzito kati ya Januari 2021 na Januari 2022.

Bw. Kipanga amesema kati ya wasichana hao, 1,554 ni wa shule za msingi na 7,457 wa shule za sekondari, na wasichana 1,692 wa shule za sekondari walirudi shuleni baada ya kujifungua.

Bw. Kipanga pia amesema serikali bado inatathmini idadi ya wasichana wa shule za msingi ambao wamerejeshwa shuleni baada ya kujifungua.