UNHCR na wadau wahitaji dola milioni 556 za kimarekani kuwasaidia wakimbizi nchini Sudan
2023-02-01 08:54:18| CRI

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR pamoja na wadau 41 wa kitaifa na kimataifa wametoa mwito wa kuchangiwa dola milioni 556 za kimarekani kuwasaidia wakimbizi wanaoishi nchini Sudan.

Shirika hilo limetoa taarifa ikisema mwito wake wa kukusanya fedha kati ya mashirika wa mwaka 2023 unalenga kuchangiwa fedha za kutoa msaada unaohitajika zaidi kwa wakimbizi zaidi ya laki 9 nchini Sudan.

Mjumbe wa UNHCR nchini Sudan Bw. Axel Bisschop amesema mpango wa kuwasaidia wakimbizi ulioendelezwa na washirika wote ikiwemo kamati ya wakimbizi ya Sudan, utatoa ulinzi muhimu na msaada wa kuokoa maisha kwa jamii za wakimbizi nchini Sudan.

Ameongeza kuwa kwa kutambua mazingira ya kimataifa ya kibinadamu na migogoro mbalimbali inayowakabili, wanaitia moyo jumuiya ya kimataifa kuunga mkono mpango wa mwitikio wa suala la wakimbizi uliotolewa hivi karibuni nchini Sudan.