Mashirika ya fedha ya kimataifa na wakopeshaji wa kibiashara ni muhimu katika kuipunguzia Zambia mzigo wa madeni
2023-02-01 08:41:07| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Mao Ning amesema njia bora ya kutatua suala la mzigo wa madeni kwa Zambia, ni ushiriki wa mashirika ya fedha ya kimataifa na wakopeshaji binafsi.

Akiongea baada ya wizara ya fedha na mipango ya Zambia kutoa takwimu kuhusu deni, Bibi Mao amesema China imetoa mchango mkubwa katika kushughulikia deni la Zambia chini ya mfumo wa kundi la G20. Ameongeza kuwa asilimia 24 ya deni la Zambia inatokana na mashirika ya fedha ya kimataifa, na wakopeshaji wa kibiashara wa magharibi ni asilimia 46.

Amesema mikopo inayotolewa na China kwa Zambia kwenye miradi kama ya nishati, inasaidia kuimarisha uwezo wa Zambia kuhimili deni, na si kinyume chake.