UM waisaidia Burundi kukabiliana na msukosuko wa tabianchi
2023-02-01 08:23:29| CRI

Timu ya Umoja wa Mataifa nchini Burundi inafanya kazi na serikali na washirika kupambana na athari kubwa za mabadiliko ya tabianchi.

Naibu msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Farhan Haq amesema, karibu asilimia 90 ya wakimbizi wa ndani 75,000 nchini Burundi wanaendelea kuhama kutokana na majanga yaliyosababishwa na mabadiliko ya tabianchi, na zaidi ya nusu yao ni wanawake.

Msemaji huyo amesema Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja Mataifa (FAO), Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Shirika la Kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa wanapambana na utapiamlo sugu, kuhimiza anuwai ya kilimo nchini humo na kuongeza mwamko wa umma kuhusu tabianchi.