Mawaziri wa ulinzi wa nchi za Afrika wanafanya mkutano wa siku mbili mjini Mogadishu, kujadili juhudi za kuleta utulivu nchini Somalia.
Waziri wa habari, utamaduni na utalii wa Somalia Bw. Daud Aweis Jama, amesema mawaziri kutoka nchi za mstari wa mbele yaani Djibouti, Kenya na Ethiopia wanatarajiwa kupitisha msimamo wa pamoja kuhusu usalama wa kikanda na mapambano dhidi ya kundi la Al-Shabaab.
Mkutano huo pia unahudhuriwa na wakuu wa majeshi, na makamanda wa nchi zinazochangia vikosi, pia utapitisha mkakati wa pamoja wa kupambana na ugaidi.
Mkutano huu ni mkutano wa utangulizi wa mkutano wa kilele utakaofanyika chini ya uenyekiti wa Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud, ambaye ataeleza hali ya jumla ya usalama nchini Somalia, na hasa operesheni dhidi ya kundi la Al-Shabaab.