Matukio mengi ya kigaidi yatokea nchini Burkina Faso
2023-02-01 23:07:45| cri

Serikali ya Burkina Faso imesema, matukio mengi ya kigaidi yametokea nchini humo hivi karibuni, na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30, wakiwemo askari na raia. Burkina Faso iko katika eneo la Sahel barani Afrika, ni nchi ambayo imekuwa ikikabiliana na vitisho vya kiusalama kama vile ugaidi.