China yatuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha waziri wa mambo ya nje wa Gabon
2023-02-02 08:34:23| CRI

Mjumbe maalum wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Bw. Liu Yuxi jana Jumatano ametembelea ubalozi wa Gabon mjini Beijing kuomboleza kifo cha waziri wa mambo ya nje wa Gabon Bw. Michael Moussa Adamo.

Kwa niaba ya China Bw. Liu ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Moussa na kutoa pole kwa familia yake.

Kaimu balozi wa Gabon nchini China Bw. Guy Arnaud Pambou Mavoungou ameishukuru China kwa kutambua mchango wa Bw. Moussa katika maendeleo ya uhusiano wa kirafiki kati ya Gabon na China na kuelezea nia ya kuendelea kufanya juhudi na China kusukuma mbele ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.