Msomi wa Afrika: Jaribio lolote la kuvuruga uhusiano kati ya Afrika na China halitafanikiwa
2023-02-02 10:48:37| CRI

Hujambo msikilizaji na karibu tena kwenye kipindi hiki cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Kipindi hiki kinakuletea habari mbalimbali kuhusu China na nchi za Afrika. Mara nyingi nchi za Magharibi zimekuwa zikijitahidi kuvuruga ama kupaka matope uhusiano na ushirikiano kati ya China na nchi za Afrika, kutokana na hilo, mtaalamu wa masuala ya kimataifa kutoka nchini Mali Prof. Yoro Diallo amesema kuwa, jaribio lolote la kuvuruga uhusiano huo kamwe halitafanikiwa, zaidi utasikia katika ripoti yetu ya leo. Lakini pia tuna mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi ambayo itahusiana na Sikukuu ya Mwaka Mpya wa Jadi wa Kichina na jinsi Wakenya na jamii ya Wachina wanaoishi nchini Kenya walivyosherehekea Sikukuu hiyo.